SERIKALI INASEMA NINI JUU YA ULAJI WA MENDE TANZANIA? SOMA HAPA - MRS. BENSON

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 2 August 2016



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

SERIKALI INASEMA NINI JUU YA ULAJI WA MENDE TANZANIA? SOMA HAPA


Baada ya utafiti wa siku chache kubaini wingi wa protini katika maziwa yanayoweza kutolewa kutoka aina mpya ya mende, Serikali imesema haina mpango wa maziwa hayo kwa sasa.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja baada ya timu ya kimataifa ya wanasayansi kubaini chembechembe za protini ndani ya mende aina ya diploptera puntuate ambaye huzaa watoto tofauti na aina nyingine.

Mratibu wa kitaifa wa uongezaji wa virutubisho katika chakula kutoka taasisi ya chakula na lishe (TFNC), Celestine Mgoba alisema “Wala hatuna mpango wa mende kwenye matumizi ya vyakula. Ni mpaka utafiti ufanyike na Serikali itoe kibali. Inawezekana tu mtu amefanya utafiti wake, ni mpaka uthibitishwe “.

“Kitu chenyewe mende? Ukiwaambia watu kuhusu ubora wa maziwa ya mbuzi tu inakuwa shida, wengi wanataka maziwa ya ng’Ombe, ndiyo utakuja kusema mende? Halafu hao mende watatoa kiasi gani, maana yatatakiwa mengi,”alisisitiza

Mratibu wa taasisi hiyo alisema licha ya kutofahamu utafiti huo., bado mende hakubaliki kwa jamii ya Watanzania kama chakula.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here