SAIKOLOJIA NI NINI HASWA? - MRS. BENSON

Breaking

Post Top Ad

SAIKOLOJIA NI NINI HASWA?

Saikilojia ni neno linalotokana na neno la kingereza (psychology) ambalo asili yake ni neno la kiyunani (psyche) lenye maana ya nafsi au roho. Kwa ujumla wake saikolojia ni sayansi inayohusu nafsi au roho na namna nafsi hii (roho) inavyo fanya kazi. Vile vile saikolojia inahusu elimu ya ufahamu wa tabia za wanyama hasa binadamu. Kwa elimu hii ya saikolojia unaweza kufahamu vyanzo vya tabia flani kwa binadamu, pia inampa binadamu uwezo wa kujielewa madhaifu yake na mazuri yake na namna bora ya kuyaepuka (madhaifu) au kuishi nayo bila kuleta madhara na namna bora ya kuyaendeleza mazuri aliyonayo.

Wataalamu wa saikolojia siku zote hupenda kufahamu kwa upana tabia za binadamu kupitia tafiti ikiwa ni pamoja na kufahamu mahitaji yake, motisha, hamasa zake, hisia zake (mwenendo wa fikra zake na mihemuko yake). Hii huwafanya wataalamu wa saikolojia kubuni njia na kutuo ushauri ambao humfanya (humuwezesha) binadamu kuishi maisha ya furaha na amani.

Saikolojia ni somo ambali haliepukiki katika maisha ya binadamu. Nikweli na ni wazi kuwa kila binadamu ni wapekee. Upekee huu unasababiswa na mambo makubwa mawili ambayo ni ASILI (Nature) na MAZINGIRA (nurture). Kutokana na mambo haya mawili, binadamu hujikuta tukitofautiana kuanzia maumbile yetu hadi tabia zetu. (hata wale ambao wanachangia baba mmoja na mama mmoja). Upekee huu pia umetufanya kuwa na utofauti wa hisia (mihemko).

Kwa kuzingatia ukweli kuwa binadamu tunategemeana ili kuendelea kuishi kwa amani na furaha na kwa mafanikio, ni wazi kwamba kutegemeana huku kunatokana na utofauti tulio nao. Jaribu kufikiri, kama binadamu wote tungekuwa na tabia moja, maumbile yanayo fanana, nguvu zinazolingana, vipaji vinavyo fanana, hisia zinazo fanana nk. Ni nani angemtegemea mwenzake?  Na kungewa na umuhimu gani wa kuwa na marafiki? Au dunia ingekuwaje? Hivyo basi ni kwa uelewa wa elimu ya saikolojia inayotuwezesha na kutusaidia kuanzisha mahusiano na kuyalinda ili tuendelee kusaidiana na kushirikiana kupitia mbalimbali za kimaisha.

Pia upatikanaji wa elimu hii ya saikolojia sio kitu kigumu kama watu wengi wanavyo dhani. Kuipata elimu hii sio lazima uhudhurie mafunzo maalumu katika chuo husika kwa sababu maisha yetu kwa asilimia kubwa yametawaliwa na elimu hii ya saikolojia. Watu wengi wamekuwa wkitumia nadharia za kisaikolojia katika maisha yao ya kila siku pasipo kufahamu. Kwa mfano: ni mara nyingi mno watu katika maisha yao ya kawaida kuanzisha mahusiano kwa malengo tofauti. Na baadhi yao wamekuwa wakifanikiwa kuanzisha mahusiano hayo huku wengine wengi wakishindwa kanzisha au hata kuyatunza. Hii ni moja ya Nyanja ya saikolojia (social psychology) ambayo inashauriwa kila mmoja kuwa nayo kwa kiasi flani.

Kupitia elimu ya saikilojia utaweza kujua namna bora ya kuishi na mwenzako wa ndoa au mchumba wako na hata rafiki yako(mpenzi). Pia kwa wale ambao wamejaaliwa kupata watoto watafahamu namna bora ya kuwalea watoto wao na huduma za msingi ambazo mtoto anastahili katika umri husika. Kwa wale wenye mogogoro katika mahusiano yao au ndoa zao, elimu hii itawapa majibu ya uhakika. Pia elimu hii inawahusu viongozi wa ngazi zote kuanzia ngazi ya familia nakuendelea… kwani kwa kupata elimu hii itakuwezesha kuwaelewa watu anao waongoza na hivyo kufanya kazi ya uongozi kuwa rahisi. Kwa wanafunzi ambao wanapenda kosoma na kufaulu kwa ngazi zote,  elimu hii ni muhimu sana kwao. Kunamambo mengi sana ambayo kwa kupitia elimu hii watu wanaweza kupata kile wanachokitafuta bila kutimia njia ambazo si rasmi kama kwenda kwa waganga wa kienyeji, nk.

Kwa kuhitimisha Elimu hii ya saikolojia ina malengo mengi na kazi nyingi katika maisha ya binadamu. Baadhi ya malengo hayo ni pamoja na kumfanya binadamu ajielewe yeye ni nani? Kwa nini yuko hivyo jinsi alivyo? Anapenda jinsi alivyo? Vitu gani avifanye na asivifanye kwa  muda husika? Afanye nini ili aachane na tabia ambayo inamkwaza yeye pamoja na watu wao mzunguka kwa mfano, uvutaji sigara, bangi, wizi nk. Pie elimu hii iana lengo la kumuwezesha binadamu kuelewa mazingira yanayo mzunguka ikiwa ni pamoja na watu wao mzunguka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here