Post Top Ad
Friday, 6 October 2017

UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA ➞




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »
Home
INJILI
MAKALA
MASOMO YA MWAKASEGE
STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAKE. - MFULULIZO WA SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAK
CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAKE. - MFULULIZO WA SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAK
Bwana Yesu asifiwe milele!
Ndani ya somo lililotangulia kabla ya hili, nilikuwa najibu swali hili: “Ikiwa umeota ndoto ambayo tafsiri yake huijui ufanyeje?”
Nilipokuwa nakupa majibu ya swali hilo, nilikufundisha vipengele vinne muhimu, katika kutafsiri ndoto. Leo – nataka nikufundishe kipengele cha tano, kitakachoweza kukusaidia katika kutafsiri ndoto unazoota, kipengele hicho ni hiki: “ANGALIA ULICHOKUWA UNAWAZA KUKIFANYA KABLA YA KUOTA NDOTO ULIYOOTA”
Waefeso 3:20 inatukumbusha ya kuwa, Mungu anaweza “kufanya mambo ya ajabu mno, kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo…”Kwa hiyo – ikiwa Mungu anatumia “ndoto” kama njia mojawapo ya kuwasiliana na watu (Ayubu 33:14,15) ina maana Mungu anaweza kutumia “ndoto” kujibu mawazo ya mtu, au kufikiri kwa mtu, au maombi ya mtu!
Ndiyo maana kwenye kipengele hiki cha tano, juu ya kutafsiri ndoto, nasisitizia umuhimu wa kuangalia ulichokuwa unawaza kukifanya kabla ya kuota ndoto uliyoota!
Hebu tujifunze jambo hili kwa mifano ifuatayo:
MFANO WA 1: YUSUFU ALIPOTAKA KUMKIMBIA MARIAMU.
Ukisoma habari iliyoandikwa katika Mathayo 1:18 – 20, utaona ya kwamba, kulikuwa na uhusiano wa kile ambacho Yusufu alikuwa anafikiria kukifanya, na ndoto aliyoota!Wakati huo Yusufu ambaye alikuwa anajiandaa kumwoa Mariamu – “akaazimu kumwacha kwa siri”, baada ya kusikia kwamba alikuwa mja mzito.
Biblia inasema; “Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema…usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”.Ni dhahiri ndoto ile aliyoota Yusufu ilikuja ili kujibu alichokuwa anafikiri kukifanya – kumwonyesha ya kuwa hakikuwa sahihi!
Yusufu aliamua au aliazimu kumwacha Mariamu, kwa kuwa hakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya mimba ya Mariamu. Ndoto ile ilimpa ufahamu, uliomsaidia kubadili kile alichokuwa anafikiria kukifanya.
MFANO WA 2: MAMAJUSI
Mamajusi waliombwa na Mfalme Herode, wampe taarifa ikiwa watajua Yesu alipozaliwa, ili naye aende kumsujudia
Ukisoma Mathayo 2:1 – 18 utajua ya kuwa si kweli kwamba Herode alitaka kujua Yesu alipozaliwa ili amsujudie – bali apate kumwua! Lakini Mamajusi hawakujua hila hizo za Herode! Kwa hiyo – walipomaliza kumsujudia Yesu na kumpa zawadi walizompelekea, wakawa wanajiandaa kurudi kwa Herode kumpa taarifa ya mahali Yesu alipokuwepo.
Ndipo biblia inasema; “Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine’ (Mathayo 2:12). Mungu aliingilia kati kwa njia ya ndoto, kuwazuia Mamajusi wasifanye kile walichokuwa wanafikiria kukufanya!
Tunaona tena katika mfano huu wa pili, umuhimu wa kufuatilia ulichokuwa unawaza – kama njia mojawapo ya kukusaidia kujua tafsiri ya ndoto uliyoota!
MFANO WA 3: KUHAMIA KANISA LINGINE
Kuna mtu aliyenishirikisha ndoto hii ifuatayo, baada ya kuamua moyoni mwake, kutaka kuhama toka Kanisa alilokuwa anasali, na kuhamia kanisa lingine – ambalo yeye aliona ni bora kuliko lile alilokuwa anasali wakati huo. Aliota ndoto ambayo ndani yake alimwona mchungaji wa Kanisa alilotaka kuhamia. Mchungaji huyo alikuwa anawaongoza waumini wake kuelekea porini – huku na yeye aliyeota ndoto hiyo akiwemo kwenye kundi hilo.
Na huko porini wakapotea njia na hawakujua pa kutokea – mchungaji wao na waumini wake. Na akaamka toka usingizini wakiwa wamepotea porini!
Mtu huyo alipoamka toka usingizini, na kuitafakari ndoto aliyoota – alijua Mungu alikuwa amemtumia ujumbe kwa njia ya ndoto aliyoota, ya kuwa uamuzi wa kuhamia kanisa alilotaka kuhamia, haukuwa sahihi! Na ikiwa ataamua kupuuza onyo lile, basi, angejikuta amepotea kiroho na kimaisha!
Yule mtu aliyeota ndoto ile, akanieleza ya kuwa aliamua kusitisha uamuzi wake wa kuhama kanisa kama alivyokuwa anataka kufanya!
Kumbuka: Njia mojawapo itakayokusaidia kutafsiri ndoto uliyoota, ni wewe kutathmini mawazo uliyokuwa unawaza kabla ya kuota ndoto uliyoota. Hii ni muhimu kwa sababu, ndoto hiyo inawezekana imeletwa kwako ili kujibu, au kurekebisha, au kuonya, au kuthibitisha - misimamo ya mawazo uliyokuwa unawaza, kabla ya kuota ndoto hiyo uliyoota!
Mungu aendelee kukubariki unapoendelea kujifunza somo hili pamoja nasi!
Ili kupata Habari, Stori, na Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta PRINCE BEWISA, au
BONYEZA HAPA

TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?
Facebook Plugin by
princebewisa
Tags # INJILI # MAKALA # MASOMO YA MWAKASEGE # STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
Share This

About Benson Mmari
Benson Mmari ni mwaandishi wa makala za mitandaoni akijikita zaidi katika kuelimisha kuhusiana na masuala ya Afya, Saikolojia, na Mahusiano - Kimwili na kiroho.
Ni mwanateknolojia aliyebobea kwenye kazi zake tangu mwaka 2012.
Newer Article
SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 5
Older Article
SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 4
SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 5
Benson MmariOct 07, 2017CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAKE. - MFULULIZO WA SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAK
Benson MmariOct 06, 2017SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 4
Benson MmariOct 05, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment