UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME WAPUNGUA KWA ASILIMIA ZAIDI YA 50 - MRS. BENSON

Post Top Ad

Monday, 18 September 2017

demo-image



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA
rlx pb%2BApp
PUSH%2BBN%2B728%2BV1

KILIHOST%2BADS
« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME WAPUNGUA KWA ASILIMIA ZAIDI YA 50

BewisaTV+Banner
spermUtafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Hebrew-Hadassah Braun, cha Mjini Jerusalem umebaini kuwa kiwango cha mbegu za kiume kwa wanaume duniani kimepungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Kwa mujibu wa utafiti huo, kiwango na ubora wa mbegu za kiume kimeshuka katika kipindi cha chini ya miaka 40 na hakuna ushahidi kuwa kiwango hicho kitaongezeka.

Utafiti huo umesisitiza kuwa kiwango na idadi ya mbegu za kiume kimeshuka zaidi kwa wanaume wa nchi za Magharibi huku pia zikidaiwa kushuka katika ubora na idadi na hivyo kuwa tishio kwa uwepo wa watu duniani.

“Utafiti huu unawapa wasomi kazi kubwa zaidi hasa kwani idadi ya mbegu za kiume na afya ya binadamu ni muhimu zaidi. Wasomi sasa wanatakiwa kuchunguza chanzo cha kushuka huko kwa idadi ya mbegu za kiume na namna ya kutatua tatizo hilo,” amesema mmoja wa watafiti hao, Dkt. Hagai Levine.

Dkt. Hagai ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira na Afya wa Chuo cha Hebrew, amefanya utafiti huo kwa kushirikiana na Profesa Hannah Swan wa Chuo Kikuu cha New York, Kitengo cha Afya ya Jamii.

Madaktari wengine waliohusika katika utafiti huo ni wa kutoka nchi za Brazil, Denmark, Israel, Uhispania na Marekani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *