MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA KIWANJA KWA AJILI YA MAKAZI - MRS. BENSON

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 30 August 2017



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA KIWANJA KWA AJILI YA MAKAZI


Hello, hujambo mtu wangu? karibu tena hapa Prince Bewisa na leo tunakudondoshea dondoo kadhaa za nini cha kufanya kabla ya kununua kiwanja ili baadae isije ikakupata shida ambayo itakupa huzuni.

Kubwa zaidi kabla ya kununua kiwanja chochote ni muhimu kujua ni kwanini unanunua eneo hilo la ardhi. Je ni kwajili ya shughuli za kilimo, nyumba ya kuishi au biashara, kiwanda n.k

Kumbuka kuwa nyumba au ardhi ni hazina kubwa hivyo hakikisha na ni sehemu sahihi ya shughuli yako. Kama ni eneo la kimakazi na unataka kujenga nyumba ya kuishi basi zingatia haya.

 -   Hakikisha muuzaji anatoa hati sahihi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi uliyoko.
 -  Hakikisha ni eneo salama na linalofikika, hapaathiriwi na mafuriko, wala mmomonyoko wa udongo. Pia pasiwe ni karibu na viwanda hatarishi kwa malezi ya watoto.
  -  Pawe karibu na huduma muhimu kama soko, msikiti au kanisa, shule, stendi ya mabasi, hospitali na huduma nyingine muhimu .
  -  Ni vema pia kuangalia Udongo wa eneo husika kama ni sahihi kwa aina ya shughuli unayotaka kufanya au nyumba unayotaka kujenga.
  -  Ni vizuri pia kujua kama ni eneo ambalo limepimwa kwa ajili ya makazi ili kuepuka kuvunjiwa nyumba yako hapo baadae na serikali pindi miradi ya maendeleo itakapopita hapo.
  -  Je, pana mvuto au mwonekano unaotaka wewe? Je kipo ndani ya bajeti yako?
  -  Vipi hali ya upatikanaji wa maji na umeme katika eneo hilo?

Ukijiridhisha vya kutosha kulingana na matakwa yako ndipo uamue kununua au kuacha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here