RAIS MAGUFULI AWAPATANISHA RUGE NA MAKONDA, TANGA - MRS. BENSON

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 5 August 2017



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

RAIS MAGUFULI AWAPATANISHA RUGE NA MAKONDA, TANGA



Undugu na upendo wa dhati ndio kila jambo hapa duniani kwa maisha ya kila mwanadamu mcha Mungu. Na hili limetiliwa mkazo leo na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Magufuli alipowapatanisha Ruge na Makonda.

Ruge Mutahaba. Picha na Maktaba yetu.
Kisaikolojia, kwa mtu muelewa ni jambo la kutia moyo sana na lenye kuleta undugu, furaha, na upendo pale tunapoona ndugu waliokuwa pamoja wanakosana na baadaye kuelewana na kusameheana.

Hili limetokea leo huko Tanga wakati wa uzinduzi wa Bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga Tanzania; ambapo rais Magufuli katika hotuba yake ilifika wakati akaamua kuwapongeza wasanii, lakini akaenda mbali na kumpongeza Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, ndugu Ruge Mutahaba kwa juhudi zake za kusisitiza uzalendo kupitia kampeni ya "ISHI NA MIMI".

Mh. Paul Makonda. Picha ya Maktaba.
Katika pongezi hizo aliamua kumwita Ruge, na pia alimuita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda, (ambao kimsingi walikukuwa na mgogoro kama ambavyo iliwahi kuripotiwa na vyombo vya habari) na kuamua kuwapatanisha.

Kulingana na aina ya blog yetu;
Kiroho, na kimsingi kabisa, hii ni hatua nzuri; lakini itakuwa nzuri zaidi kama msamaha huu utakuwa wa kweli kwa kila mmoja kumsamehe mwenzake toka kwenye kilindi cha  moyo wake.

HUWEZI KUSAMEHEWA KAMA HUTASAMEHE. HONGERENI VIONGOZI WETU KWA MAHUBIRI HAYA. HUU NI MFANO HAI KWETU.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here