Post Top Ad
Friday, 1 September 2017

UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA ➞




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »
Home
AFYA
MAKALA
STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
MATUNDA UNAYOPASWA KULA NA VITU USIVYOPASWA KUFANYA WAKATI WA HEDHI
MATUNDA UNAYOPASWA KULA NA VITU USIVYOPASWA KUFANYA WAKATI WA HEDHI
Mzunguko wa hedhi ni mzunguko wa kila mwezi ambao mwanamke huupata, hali ambayo huleta kutokwa na damu kutokana na mimba kutotungwa.
Kwa hali ya kawaida hedhi ya kwanza hutokea katika umri wa miaka 12 -13 na kuendelea na hutokea pale ambapo tishu za ukuta wa mji wa mimba zinapobomoka na kutoka kama damu ukeni.
Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au ki taalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.
Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation.
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili. Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni
Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
Magonjwa pia husababisha mwanamke kusikia maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo.
Leo ninayo orodha ya matunda ambayo yakitumika huweza kupunguza ma umivu wakati wa kipindi hicho.
Matunda hayo ni:-
NANASI
Hili ni miongoni kati ya matunda yenye uwezo wa kupunguza maumivu hayo yatokanayo na mzunguko wa hedhi, hii ni kutokana na tunda hili kuwa na virutubisho vyenye uwezo wa kuifanya misuli ya sehemu za siri za kike kuwa huru (kurelax) na hivyo kupunguza uwezekano wa maumivu makali.
NDIZI
Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa umuhimu wa matunda nadhani utakuwa umewahi kusikia kuhusu umuhimu wa ndizi hata kwa wanamichezo na imekuwa ikiwasaidia kurekebisha misuli na kuondoa tatizo la kukaza kwa misuli mara baada ya mazoezi, hivyo basi tunda hili pia huweza kuwasaidia wanawake ambao wanapatwa na maumivu makali wakati wa hedhi na kupunguza au kuondoa hali hiyo kabisa.
Pamoja na kukueleza kuwa matunda hayo huweza kupunguza maumivu wakati wa mzunguko lakini ni vyema kuzingatia kuwa matunda hayo yanapaswa kuliwa angalau siku mbili au moja kabla ya kuingia kwenye mzunguko wako ili kupata matokeo mazuri zaidi.
Pia unashauriwa kunywa tangawizi kila siku mara mbili, wiki moja kabla ya kupata mzunguko wako, pia maji ya kutosha kipindi cha mzunguko kwani nayo huwa na nafasi kubwa ya kusaidia kupunguza kiwango cha maumivu hayo.
Papai bichi lililokomaa husaidia kupunguza maumivu ya hedhi unashauriwa kulila mara kwa mara. Mboga za majani pia ni msaada mkubwa kwa kupunguza maumivu.
Hiki ni kichocheo na hutolewa kwenda kwenye ukuta wa kizazi kusaidia kushusha ukuta uliotengenezwa na kuandaliwa kwa kutungisha na kuimarisha mimba kumong’onyoa ukuta huo ili ukuta mwingine utengenezwe ili yaanze maandalizi mapya ya mzunguko unao fuata.
Inapotokea kuwa kiwango hiki cha Prostaglandini kinakuwa kingi kupita kiasi kinasababisha kule kukuza na kusinyaa kwa misuli ya mfuko wa kizazi kuwa kwa kiwango cha juu na wenye kuambatana na maumivu makali sana isivyo kawaida.
JIHADHARI NA VYAKULA
Moja ya baadhi ya vitu vinavyo sababisha kiwango cha Prostaglandini kuwa juu kupita kiasi ni ulaji wa vyakula vinavyo sababisha mchakato mwilini mwako na kuvuruga utendaji kazi wa mwili wako na hatimaye kuvuruguka shughuli zingine.
Vyakula hivyo ni kama vile vyakula vyenye kiwango kikubwa cha ngano, kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi na rangi kama juisi na soda ambavyo ni kemikali za viwandani. Matumizi ya pombe, kahawa, caffeine zote hivyo ni hatari sana kwa afya ya mwanamke wakati wa mzunguko wake wa hedhi.
Jiepushe kuwa na uzito kupita kiasi ndiyo maana asilimia kubwa ya wanawake wenye matatizo haya ya maumivu ya tumbo la hedhi huwa wana dalili zinazoambatana na matatizo mengine ya mfumo wa chakula kama choo kuwa ngumu, Hemmorhoids (bawasili), tumbo kuuma/kujigawa na kadhalika.
Hivyo basi unatakiwa pia kuhakikisha huna mchakato wowote unaoendelea kwenye mfumo wa chakula ili uweze kutibu tatizo hilo. Hivyo ndivyo baadhi ya visababishi vya msingi vinavyosababisha Proglandini kuwa katika kiwango cha juu sana na kusababisha misuli ya mfuko wa kizazi kukaza kupita kiasi kwa kuambatana na maumivu makali hasa wakati wa hedhi.
Kuna wanawake wengine wanakuwa na matatizo ya kiafya katika mfumo wa uzazi ambayo sasa yanasababisha hedhi mbovu kwa mwanamke. Aina hii ya kisababishi huitwa kisababishi sekondari, jina hili linatokana na jinsi dalili za hedhi mbovu zinavyotokea baada ya mwanamke kuwa na matatizo ya kuwa hedhi mbovu kwa kuwa na sekondari ya ugonjwa katika mfumo wa uzazi. Magonjwa haya yanaweza kuwa kama Endometriosisi .
Huu ni ugonjwa ambao haujulikani kuwa unasababishwa na nini hadi sasa lakini hauwezi kuambukizwa hata kwa kutumia njia ya kujamiana, huu ugonjwa unasababishwa na zile seli za ukuta wa mfuko wa kizazi zinatoka zinaenda kujipandikiza popote nje ya mfuko wa kizazi na kuwa na sifa ile ile kama zinapokuwa ndani ya mfuko wa kizazi.
Mbali na endometriosisi pia hedhi mbovu kama dalili ya msingi inaweza kusababishwa na vimbe ambazo zinaota ndani ya mfuko wa kizazi, nje ya mfuko wa kizazi na kwenye misuli ya kizazi ambazo huita fibroids.
Wagonjwa wengi yenye fibroids hulalamika kupata hedhi mbovu.Wanawake wengine huchanyama maumivu wanayo pata wakati wa hedhi na maumivu ya maambukizi kwenye mirija ya uzazi yani PID (Pelvic Inflammatory Diseases) hii ni kwa sababu inaweza kuwa ulipata maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanzo halafu maambukizi hayo yakapanda hadi kwenye mirija ya uzazi na hatimaye kusababisha dalili hizo za kiuno kukaza na kuuma sana lakini ukitaka kutofautisha tatizo hilo zingatia kwamba maumivu yanayotokana na PID hayaambatani na siku za hedhi hivyo ndivyo unaweza kutofautisha kiurahisi kabisa.
Shaloom!
Ili kupata Habari, Stori, na Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta PRINCE BEWISA, au
BONYEZA HAPA

TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?
Facebook Plugin by
princebewisa
Tags # AFYA # MAKALA # STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
Share This

About Benson Mmari
Benson Mmari ni mwaandishi wa makala za mitandaoni akijikita zaidi katika kuelimisha kuhusiana na masuala ya Afya, Saikolojia, na Mahusiano - Kimwili na kiroho.
Ni mwanateknolojia aliyebobea kwenye kazi zake tangu mwaka 2012.
Newer Article
FAHAMU MAANA YA SAIKOLOJIA
Older Article
UNAPASWA KUJIPONGEZA MWENYEWE LEO. SABABU HIZI HAPA
SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 5
Benson MmariOct 07, 2017CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAKE. - MFULULIZO WA SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAK
Benson MmariOct 06, 2017SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 4
Benson MmariOct 05, 2017
Labels:
AFYA,
MAKALA,
STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment