MADHARA YA KULA NYAMA NYEKUNDU - MRS. BENSON

Post Top Ad

Monday, 18 September 2017

demo-image



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA
rlx pb%2BApp
PUSH%2BBN%2B728%2BV1

KILIHOST%2BADS
« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

MADHARA YA KULA NYAMA NYEKUNDU

BewisaTV+Banner
nyama+nyekunduUtafiti unaonyesha ulaji wa nyama nyekundu una madhara makubwa sana kuliko ulaji wa nyama nyeupe. Hata hivyo watu ambao hawali nyama kabisa wako mbali sana na hatari hizi. 

Lakini kwa kula nyama pia ina faida katika miili yetu na nyama nyeupe ni salama sana kuliko nyekundu.
Haya ni baadhi ya madhara ya ulaji nyama hiyo:

1. Hatari ya kupata magonjwa ya moyo:
Nyama ina kitu kinaitwa lehemu, kitaalamu inajulikana kama cholesterol, hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri.
Hii husababisha viuongo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kazi. Japokua cholesterol ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha hii inayoongezeka kutoka kwenye nyama ni hatari sana.
[nyama nyekundu ina cholestrol nyingi zaidi]

2. Kansa ya utumbo mkubwa:
Nyama nyekundu ikiliwa inakaa masaa ishirini kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine. Utafiti unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara haya yameonekana kutokuwepo kwa kula nyama nyeupe.

3. Ugonjwa wa kisukari:
Watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa kisukari sana kuliko wale wasiokula; na hii ni baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka kumi mfulululizo [cohort studies]

4. Ugonjwa wa kifafa:
Minyoo inyopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa. Halii hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.

5.Unene uliopitiliza:
Nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo na hii hupelekea wao kupata unene; jambo ambalo ni hatari sana kwani husababisha matatizo mengi ya kiafya

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *