FAHAMU MBINU ZITAKAZOKUWEZESHA KUPATA AJIRA KIRAHISI - MRS. BENSON

Post Top Ad

Wednesday, 20 September 2017

demo-image



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA
rlx pb%2BApp
PUSH%2BBN%2B728%2BV1

KILIHOST%2BADS
« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

FAHAMU MBINU ZITAKAZOKUWEZESHA KUPATA AJIRA KIRAHISI

BewisaTV+Banner
AjiraLeo ningependa tuzungumzie mbinu za kutafuta na kupata kazi kirahisi kutokana na ukweli kwamba wengi wanahitaji fursa hiyo.

Kimsingi kuna maangalizo mengi katika mada hii ambayo watu wasiokuwa na ajira wanatakiwa kuzingatia lakini kwa uchache tutaangalia yale ambayo ni muhimu kufuatwa na watafuta ajira ili waweze kufanikiwa kirahisi na kuepuka madhara ya kisaikolojia na kutopata kazi.

Ni ukweli usiofichika kwamba hakuna jambo muhimu maishani kama kuwa na kazi inayokuingizia kipato.

Hata hivyo, ni lazima pia tukubaliane kwamba si kazi nyepesi kupata kazi. Sote ni mashahidi wa jinsi watu wanavyohangaika mitaani kutafuta kazi, hata kama wamesoma na wana ujuzi wa kutosha.

Sote ni mashahidi pia wa jinsi baadhi ya watu wanavyochanganyikiwa wanapoishi muda mrefu bila kuwa na kazi.

Wengi hupatwa na vichaa na wengine kujiingiza katika ulevi wa kupindukia na utumiaji dawa za kulevya kutokana na kukata tamaa ya maisha kwa kukosa kazi.

Hii inatokana na watu wengi kukosa elimu ya namna wanavyoweza kutumia vizuri muda wao wa dhahabu wanapokuwa hawana kazi kwa sababu mkosa ajira huathirika endapo atashindwa kutumia muda wa awali kujiokoa na makucha ya kukosa kazi.

Ni rahisi kupata kazi muda mfupi baada ya kumaliza shule au kufukuzwa kazi kuliko kukaa nje ya ajira (kijiweni) kwa miaka sita au saba.

AMINI
Umewahi kukaa kitako na mtu yeyote aliyefanikiwa na ukamuuliza siri ya mafanikio yake? kama haujawahi kufanya hivyo mimi nimefanya utafiti kwa niaba yako kupitia watu zaidi ya 100 waliofanikiwa, kati ya mambo makuu niliyojifunza kutoka kwao la kwanza ni Imani. Hebu ngoja kwanza kwa maana nimeanza kuzungumzia imani naona mtu kafunga opera mini yake, sikupeleki kanisani bali nazungumzia imani juu ya matendo na mipango yako binafsi, ukitaka mafanikio ya kitu chochote huna budi kuikumbatia imani ni rafiki pekee ajuaye kutia moyo, kufariji na kamwe hatoacha kuyavutia mafanikio mifuko mwako. Amini kuwa utapata ajira hata kama mazingira hayaruhusu na hakuna dariri yoyote ya wewe kufanikiwa, na kama ukiandamwa na wasiwasi chukua uamuzi mgumu jisemee moyoni au hata kwa sauti “Naamini nitapata ajira, Naamini nitafanikiwa – huu ni wasiwasi tu – unataka nikate tamaa – sikubali, sitokata tamaa, NAAMINI NITAFANIKIWA” kwa kuamini na kwa kufuata mbinu zingine zinazofuata hapa chini NAAMINI UTAPATA AJIRA YAKO.

TULIZA AKILI
Inashauriwa kuwa muda mfupi baada ya kufutwa kazi au kumaliza masomo na kukutana na vikwazo vya awali vya kukosa kazi, mhusika hatakiwi kuwa na taharuki kwa kuanza kunywa pombe, kustarehe, kuwa na msongo wa mawazo, bali anatakiwa kutulia na kuendelea kushikamana na wafanyakazi wenzake wa awali, wanafunzi waliomaliza naye shule na watu ambao wako kwenye mtandao wa kazi ili kujiweka katika mazingira ya kuokoka ndani ya muda muafaka.

JITAMBUE
Mkosa ajira anatakiwa kujitambua kuwa yeye ni nani na kuhakikisha kuwa maisha yake yanakwenda kama yeye alivyo. Mhusika anatakiwa kutunza kumbukumbu zote za elimu yake kama vyeti na kuwa hai kila siku katika ujuzi wake. Pia haifai kuwa na aibu kwa kujiona duni, ni vema kuwa na imani kuwa kipindi cha kukosa ajira ni cha muda mfupi.

JITAMBULISHE
Muda wa awali ambao mtu atakuwa hana kazi ni muhimu sana kwake kufanya utambulisho kwa rafiki zake, ahakikishe kuwa watu wanaweza kuwasiliana naye kwa urahisi. Si busara kujifungia chumbani na kuzima simu, kufanya hivyo kunaweza kuwafanya rafiki zako washindwe kukupa dokezo za nafasi za kazi na hata kukusahau kabisa.

JIWEKE TAYARI
Unapokuwa huna ajira ni lazima uwe tayari wakati wote kwa kuanza kazi, isiwe unaambiwa kazi imepatikana unaanza kusema “sina vyeti, viko kwa bibi” muda wa dhahabu lazima utumike vizuri ili kutopoteza muda wa kujikomboa. Ni muhimu pia kuandaa CV yako na kuwa nayo kwenye kabati ili itakapohitajika usipoteze muda kuiandaa!

USIULEMAZE MWILI
Kuna watu ambao huchelewa kuamka au kushinda wamelala kwa sababu hawana kazi za kufanya, jambo ambalo ni hatari kwa afya. Hata kama ukosefu wa ajira unakuumiza kiasi gani usikubali kubweteka kwa kulala, utumikishe mwili pengine hata kwa kazi ambazo si za masilahi makubwa. Haifai kulazimisha sana ajira kwa kuwaganda mabosi.

USIKATE TAMAA
Kifupi hatua hizi ni muongozo wa kuweza kutumia muda wa dhahabu katika kupata kazi, hata hivyo mtu hatakiwi kukata tamaa ya kutafuta kazi ingawa ukweli utabaki kuwa kadiri unavyozidi kuchelewa kupata kazi kwa miaka mingi ndivyo anavyozidi kuweka mazingira magumu ya kuajiriwa. Hivyo ni bora ukahangaika mapema kwa kutumia uwezo na mbinu zote ili kuepuka kupotea katika ulimwengu wa ajira na kujikuta umeathirika kisaikolojia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *