SAKATA LA LEMA KUBAGULIWA MSIBANI JANA LAFIKA BUNGENI - MRS. BENSON

Post Top Ad

Tuesday, 9 May 2017

demo-image



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA
rlx pb%2BApp
PUSH%2BBN%2B728%2BV1

KILIHOST%2BADS
« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

SAKATA LA LEMA KUBAGULIWA MSIBANI JANA LAFIKA BUNGENI

BewisaTV+Banner
LEMA+BUNGENIWabunge wawili wa Chadema, Peter Msigwa wa Iringa Mjini na Godbless Lema wa Arusha Mjini wameomba mwongozo wa Spika kuhusu ubaguzi wa kisiasa uliotokea kwenye msiba mjini Arusha Jumatatu.

Jana Jumatatu jijini Arusha ilikuwa inaagwa  miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha katika ajali ya gari.

Wa kwanza kusimana alikuwa Msigwa ambaye amehoji kama ni haki kutowapa fursa Meya wa Arusha, Calist Lazaro na Mbunge wa jimbo hilo, Lema kutoa salamu za rambirambi.

Lema kwa upande wake amesema hata magari mawili ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na yeye na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari yaliondolewa kwa sababu yana majina yao.

Amesema ni kwa sababu walimheshimu makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vinginevyo mambo kama hayo huwa hayatokei mbele yao.

Mwenyekiti wa Bunge  Najma Giga amesema atatoa mwongozo huo baadaye.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *