Post Top Ad
Monday, 4 September 2017

UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA ➞




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »
FAIDA YA KULA UGALI WA DONA
Watu wengi (bila shaka hata wewe msomaji wa makala haya), hawako tayari kutumia unga usiokobolewa maarufu kama dona. Kuwalazimisha watu wa aina hiyo kutumia unga usikobolewa (unga wa dona) ni sawa na kuwaweka watu hao katika hatari ya kuwa na lishe duni.
UNGA WA MAHINDI
Unga wa mahindi, ulezi, uwele, mtama na kadhalika ni chanzo kikubwa kwa watu wengi barani Afrika cha virutubisho kama vile wanga, protini, madini na vitamini. Hata hivyo, namna ya usagaji na matumizi ya unga wa mahindi na nafaka hizo inaweza kuukosesha mwili faida ya virutubisho vilivyomo katika nafaka hiyo.
UNGA ULIOKOBOLEWA
Mahindi yaliyokobolewa yaani sembe au nafaka zingine zikikobolewa kama mtama, ulezi n.k hupoteza sehemu fulani ya nafaka hizo. Kama mahindi au mtama na ulezi utasagwa bila kukobolewa unga wake huitwa unga wa dona (whole-grain flour). ambapo unga uliokobolewa kwa lugha ya kigeni unaitwa “refined flour.” Kwa upande wa mpunga kama utaondolewa ganda lake gumu la nje na bila kuung’arisha, mchele huo kwa kimombo utaitwa “brown rice.”
Na kama utang’arishwa zaidi unatitwa “polished rice” au Waswahili huita mchele super. Mchele mzuri kwa afya ya binadamu ni ule brown rice japokuwa wengi hupendelea ule wa super.
FAIDA YA UNGA WA DONA
Unga wa dona ni unga usiokobolewa. Aina hii ya unga ina faida kadhaa, kama vile:
watu wengi kutokana na kuwa na ladha nzuri na rangi ya kuvutia.
Madini ya chuma na zinc yaliyomo kwa wingi katika nafaka mbalimbali yanaweza kutumika kwa kiwango kikubwa mwilini kama mtu atakula chakula kilichopikwa kutokana na unga uliokobolewa.
Hii ni kwa sababu nafaka zina kemikali inayoitwa “phytate” ambayo inauzuia mwili kunyonya madini hayo kutumika mwilini. Ukikoboa nafaka kama vile mahindi unapunguza kiasi kikubwa cha kemikali hiyo ya “phytate”.
FAIDA NA HASARA
Tumeona kuwa ukikoboa nafaka kama vile mahindi unapoteza baadhi ya virutubisho kama vitamini, madini na nyuzi nyuzi. Inashauriwa kwa mtu anayekula chakula kilichopikwa kutokana na unga uliokobolewa, ale na matunda na mboga za majani za kutosha ili Mosi, kiuchumi ukisaga mahindi au nafaka zingine bila ya kukoboa unapata unga mwingi kwa kila kilo utakayoisaga.
Hivyo ifahamike kuwa kukoboa kunapoteza kiasi fulani cha unga. Pili, unga usiokobolewa una kiasi kikubwa cha mafuta, protini, madini, vitamini, na nyuzinyuzi (fibre) hivyo, unaimarisha zaidi lishe ya mlaji mwilini.
Kama watu watajenga tabia ya kula mahindi ya kuchoma, kuchemsha au kupika kande pia wanapata faida kubwa ikiwemo kupata haja kubwa katika mtiririko unaofaa. Tatu, kuandaa unga usiokobolewa ni kazi rahisi katika ngazi ya familia. Nne, mara nyingi unga usiokobolewa bei yake ni nafuu. Unga uliokobolewa nao una faida zake kadhaa.
UNGA ULIOKOBOLEWA
Unga uliokobolewa unapendwa na Ugali wa dona na faida zake mwilini You are What you Eat. kuziba pengo la virutubisho vilivyopotea wakati wa kukoboa. Kwa mtu anayeweza kutumia unga usiokobolewa yaani dona, ni muhimu kwake kufanya hivyo kwa sababu faida zake ni nyingi zaidi.
USHAURI MUHIMU
Kumbuka kusaga kiasi kidogo au nunua kiasi kidogo cha dona, ili usiharibike kutokana na kukaa sana kabla ya kupikwa. Kwa upande wa mchele, watu wanashauriwa wasiukoshe sana wakati wanataka kuupika, watumie muda mfupi kuukosha ili wasile makapi.
Ni vema chakula hicho kikaliwa na matunda aina mbalimbali ili kukamilisha lishe inayotakiwa, matunda yapo ya aina nyingi. Ni muhimu kula matunda dakika 30 baada ya kula chakula.
Ili kupata Habari, Stori, na Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta PRINCE BEWISA, au
BONYEZA HAPA

TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?
Facebook Plugin by
princebewisa
Tags # AFYA # STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
Share This

About Benson Mmari
Benson Mmari ni mwaandishi wa makala za mitandaoni akijikita zaidi katika kuelimisha kuhusiana na masuala ya Afya, Saikolojia, na Mahusiano - Kimwili na kiroho.
Ni mwanateknolojia aliyebobea kwenye kazi zake tangu mwaka 2012.
Newer Article
NAMNA YA KUOMBA VIZURI NA MUNGU KUJIBU MAOMBI YAKO
Older Article
UTAJUAJE KAMA HAKUTAKI? MAJIBU
SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 5
Benson MmariOct 07, 2017CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAKE. - MFULULIZO WA SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAK
Benson MmariOct 06, 2017SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 4
Benson MmariOct 05, 2017
Labels:
AFYA,
STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment