Post Top Ad
Saturday, 16 September 2017

UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA ➞




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »
Home
AFYA
MAKALA
MAPENZI & MAHUSIANO
STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
JINSI YA KUFANYA UNAPOKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA GHAFLA
JINSI YA KUFANYA UNAPOKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA GHAFLA
KISA: Masanja na mke wake Saumu wameishi kwenye ndoa kwa miaka kumi sasa. Hapo awali, kila kitu kilikuwa sawa katika uhusiano wao, lakini katika miaka ya karibuni, Masanja amekuwa hana matamanio tena na Saumu; hana hamu kabisa ya tendo la ndoa.
FAHAMU: Tatizo kama hili la Masanja limekuwa likiwaathiri watu wengi hapa nchini na hata duniani kote. Mbaya zaidi haliwaathiri wanaume pekee kama ilivyo kwa Masanja, bali hata wanawake.
Utafiti uliofanyika nchini Uingereza, Ulaya na Marekani, ukijumuisha wanawake wa rika zote, ulibaini kuwa asilimia kati ya 30 na 50 ya wanawake wanakumbwa na tatizo la kukosa hamu ya kujamiiana.
Wakati huo utafiti huo ukiweka bayana hilo kutokana na tatizo la uzazi au kukoma kwa hedhi, tafiti nyingne zinaonyesha kuwa karibu robo tatu ya wanawake hawafikii kilele cha tendo hilo au wanapata maumivu. Nadhani unanielewa vizuri mtu wangu.
SASA TIBA IKO HIVI;
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kukosa hamu ya tendo la ndoa kunatibika, iwapo hatua muhimu na za msingi zitachukuliwa.
Ni vyema kufika mapema katika huduma za afya ukiwa na mwenza wako kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Nini suluhisho la kukosa hamu ya kujamiiana?
Kwanza kabisa, inashauriwa kitaalamu kubadilisha mfumo wa maisha kwa mfano, kubadili ratiba za kazi, matembezi au ratiba za wenza.
Kingine ni kufanya mazoezi mara kwa mara kwa sababu mazoezi huongeza ufanisi, lakini pia kupunguza uzito na humfanya mtu kuwa na umbile zuri, furaha na kuongeza ufanisi wakati wa kujamiiana.
Kupunguza msongo wa mawazo kwa kukubali kwamba tatizo lipo baina ya wanandoa na hivyo kutafuta suluhu pamoja na kuacha ugomvi. Matatizo ya kimaisha lazima yatafutiwe ufumbuzi.
Kufanya mazoezi ya misuli ya kiuno kwa kufanya kama unazuia mkojo wakati unahisi haja ndogo na kuhesabu kutoka moja hadi tano, baada ya tano pumzika na halafu rudia. Haya mazoezi (kegel exercise) huongeza uwezo wa kujamiiana kwa wanawake
Unaweza kufahamu mazoezi zaidi ya namna ya kufanya uume wako uwe na nguvu na pia uwe na hamu zaidi kwa kubonyeza HAPA.
Asante sana mdau.
Ili kupata Habari, Stori, na Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta PRINCE BEWISA, au
BONYEZA HAPA

TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?
Facebook Plugin by
princebewisa
Tags # AFYA # MAKALA # MAPENZI & MAHUSIANO # STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
Share This

About Benson Mmari
Benson Mmari ni mwaandishi wa makala za mitandaoni akijikita zaidi katika kuelimisha kuhusiana na masuala ya Afya, Saikolojia, na Mahusiano - Kimwili na kiroho.
Ni mwanateknolojia aliyebobea kwenye kazi zake tangu mwaka 2012.
SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 5
Benson MmariOct 07, 2017CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAKE. - MFULULIZO WA SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAK
Benson MmariOct 06, 2017SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 4
Benson MmariOct 05, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment