- Kubadilika rangi kwa mkojo(mfano damu katika mkojo au kwenda haja ndogo mara kwa mara)
- Uchovu na kukosa nguvu
- Maumivu ya mgongo hasa juu ya kiuno usawa wa figo
- Kuvimba miguu au mikono
- Ukosefu wa umakini na ufafanuzi wa akili
- Kukosa hamu ya kula na kutokuwa na ladha katika kinywa
- Kushindwa kupumua vizuri
- Upele au chronic tingling
Post Top Ad
Saturday, 16 September 2017

UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA ➞




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »
Home
AFYA
MAKALA
STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
DALILI ZA MAGONJWA YA FIGO NA NAMNA YA KUCHUKUA TAHADHARI
DALILI ZA MAGONJWA YA FIGO NA NAMNA YA KUCHUKUA TAHADHARI
U hali gani mtu wangu, karibu sana kwenye makala hii; aidha unatumia web au app, wote nawapa salaam na leo ninawaletea hii inayohusu FIGO.
Figo zina majukumu muhimu sana katika mwili wa binadamu - kwanza inaondoa sumu kutoka kwenye mwili wa binadamu na kusafisha damu.
Ndugu mdau wa www.princebewisa.com, ni vema ukifahamu kuwa, kama figo ya binadamu haifanyi kazi vizuri, basi hii inaweza kusababisha mkusanyiko wa sumu katika mwili na inaweza kusababisha baadhi ya matatizo makubwa ya afya.
Je, kazi za figo ni zipi haswa?
1. Kuweka katika uwiano mzuri kiwango cha maji.
Figo ina uwezo wa kusawazisha kiwango cha maji katika mwili wa binadamu, na pia inashiriki katika kutoa kemikali kwa njia ya mkojo.
2. Kutoa taka mwilini.
Sisi sote tunajua moja ya kazi kuu za figo ni kusafisha mwili, kutoa sumu, chumvi, na urea. Rejea topic ya Excretion (somo la Biology) ulipokuwa kidato cha tatu - mliobahatika kusoma.
3. Kusimamia kanuni za damu.
Kama kiwango cha oksijeni kitakuwa chini katika figo, itasababisha kuundwa kwa erythroprotein, homoni ambayo inachochea marrow [uroto] katika mifupa (bone marrow).
4. Kusimamia Kanuni za asidi.
Hii ni muhimu sana katika kazi za figo, figo zinawajibika kwa kuweka uwiano sawa wa asidi katika
mwili wa binadamu
Magonjwa ya figo.
Kuna sababu nyingi tofauti zinazoweza kukusababishia ugonjwa wa figo na kushindwa kufanya kazi, magonjwa kama kisukari, UKIMWI na shinikizo la damu.
Tunaweza kusema shinikizo la damu ni moja ya sababu ya ugonjwa wa figo na hii ndio maana inapaswa kujaribu kuweka sukari katika damu na BP katika uwiano wa kawaida.
Dalili za mwanzo za ugonjwa wa figo
Kwa bahati mbaya dalili za ugonjwa wa figo zinaanza kuonekana katika hatua za mwisho za ugonjwa, au wakati figo zinakaribia kabisa kushindwa au wakati ambao kuna protini nyingi katika mkojo.
Kwa kawaida dalili za awali za matatizo ya figo haziwezi kugundulika; ni asilimia 10 tu ya watu wanaweza kujua kama wana ugonjwa wa figo. Hata hivyo hizi ni baadhi ya ishara za mwanzo za figo kushindwa kufanya kazi.
Jinsi ya kuzuia ugonjwa wa figo na kuboresha kazi ya figo yako.
Kama tulivyosema awali, magonjwa ya figo yanaweza kukuletea matatizo makubwa zaidi katika afya zetu. Inatupasa kufanya mabadiliko katika milo yetu na mtindo wa maisha kwa ujumla.
Kipi cha kubadilisha katika mlo?
Chakula chako kisiwe na mafuta mengi, zuia utumiaji kupita kiasi wa chumvi na potassium, na upendelee kula matikiti maji au apples (matofaha), na katika chakula chako kiwe na kiwango kidogo cha protein. Pia matumizi ya maji yawe si chini ya glasi nane kila siku.
Mfumo/mtindo wa maisha.
Pendelea kufanya mazoezi hili kuweka uzito wako vizuri na kupunguza uwezekano wa kupata kisukari,na utapiamlo. Na pia zuia matumizi ya pombe na kuacha sigara.
SHALOOM
Ili kupata Habari, Stori, na Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta PRINCE BEWISA, au
BONYEZA HAPA

TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?
Facebook Plugin by
princebewisa
Tags # AFYA # MAKALA # STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
Share This

About Benson Mmari
Benson Mmari ni mwaandishi wa makala za mitandaoni akijikita zaidi katika kuelimisha kuhusiana na masuala ya Afya, Saikolojia, na Mahusiano - Kimwili na kiroho.
Ni mwanateknolojia aliyebobea kwenye kazi zake tangu mwaka 2012.
Newer Article
FAHAMU: NGONO KWA NJIA YA MDOMO HUSABABISHA SARATANI YA KOO
Older Article
JINSI YA KUFANYA UNAPOKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA GHAFLA
SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 5
Benson MmariOct 07, 2017CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAKE. - MFULULIZO WA SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - CHAKUFANYA IKIWA UMEOTA NDOTO AMBAYO HUJUI TAFSIRI YAK
Benson MmariOct 06, 2017SOMO: MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA. - SEHEMU YA 4
Benson MmariOct 05, 2017
Labels:
AFYA,
MAKALA,
STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment