UFISADI WIZARA YA NISHATI NA MADINI ULIWAHI KUELEZWA NA UPINZANI LAKINI CCM WAKAPUUZA - DED - MRS. BENSON

Post Top Ad

Thursday, 25 May 2017

demo-image



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA
rlx pb%2BApp
PUSH%2BBN%2B728%2BV1

KILIHOST%2BADS
« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

UFISADI WIZARA YA NISHATI NA MADINI ULIWAHI KUELEZWA NA UPINZANI LAKINI CCM WAKAPUUZA - DED

BewisaTV+Banner
MNYIKAJOHN JOHN MNYIKA WAZIRI KIVULI WA NISHATI NA MADINI KWA NIABA YA KAMBI RASIMI YA UPINZANI ALIELEZA KUHUSU UFISADI KATIKA NISHATI NA MADINI. CCM NA SERIKALI YAKE WALIMPUUZA NA KUKEJELI. LEO WANAOGELEA KATIKA MAMBO WALIYO KATAA
Rais John Magufuli aliunda Tume ya uchunguzi kuhusu usafirishaji wa mchanga wenye madini na ripoti imewasilishwa leo 24/05/2017 Ikulu jijini Dar Es salaam
Lakini pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa jambo hilo la kizalendo, niseme kwamba amechelewa Sana.
Kambi ya Upinzani kupitia waziri kivuli wa nishati na Madini Kamanda John John Mnyika aliwasilisha hoja binafsi kuitaka Serikali ya Ccm akiwepi Rais Magufuli akiwa waziri kuwasilisha mikataba yote ya madini bungeni na wabunge kuipitia na kuichambua kwa kina na kuifanyia marekebisho ya haraka kwa maslahi ya nchi yetu.
Wabunge wa CCM kwa kauli moja walikataa hoja hiyo ya Upinzani mwaka 2012 na mwaka 2013 kwa maslahi ya CCM. Walikataa hoja ya kuitaka Serikali kuweka hadharani mikataba na hivyo waliilinda serikali yao ya CCM kwa hofu ya kuwajibishwa.
Zitto Kabwe aliwahi kuhoji kuhusu usafirishaji wa mchanga nje ya nchi na mrahaba hafifu miaka ya 2007 ,2008 na 2009.Zitto aliibua kashfa ya Ufisadi ya Buzwagi akishirikiana na aliyekua katibu mkuu wa CHADEMA na mbunge wa Karatu Dk Slaa kwa niaba ya Kambi ya Upinzani. Spika wa bunge na bunge lilimfukuza Zitto Kabwe Bungeni kwa hoja kwamba amepotosha Bunge na Taifa badala ya kufanya utafiti na uchunguzi wa kina.
Upinzani hufikiria na kuona miaka 50 mbele wakati CCM huona kesho. Haya ya Leo Upinzani uliyasema na kuyaibua kwa vielelezo lakini Upinzani ulitukanwa kwamba nyaraka hizo ni za kufungia maandazi.
Ccm, wabunge wa CCM na Serikali ya Ccm acheni kusimamia maslahi ya CCM. simamieni maslahi ya Taifa kwa kizazi cha Leo na kesho.
danielezekiel2222@gmail.com 
ILEJE

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *