Post Top Ad
Wednesday, 16 August 2017

UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA ➞




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »
SAMAKI HAWASAHAU
Mtu huambiwa ana akili ya kusahau kama samaki. Lakini sasa huenda hilo likabadilika baada ya wanasayansi kugundua kwamba, kinyume na imani hiyo, baadhi ya samaki wanaweza kuhifadhi taarifa kuhusu mazingira waliomo kwa takriban wiki mbili.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha MacEwan, waliwazoezesha baadhi ya samaki wa Kiafrika wajulikanao kama cichlids, kuingia katika eneo maalum la tangisamaki ili kupata chakula.
Walitolewa na siku kumi na mbili baadaye walirudishwa tena ndani ya tangi samaki hilo, na saamki hao walionekana kuipendelea sehemu hiyo maalum waliokuwa wakipewa chakula.
Baadhi ya samaki wanaweza kukumbuka mazingira yao kwa muda wa wiki mbili.
Watafiti hao wanasema ongezeko hilo la muda wa samaki kukumbuka, huenda likampa samaki nafasi ya kuishi zaidi hususan wakati kuna upungufu wa chakula.
"Samaki wanaoweza kukumbuka mahali chakula kilipo, wana uwezo wa kuishi zaidi kuliko wale ambao hawakumbuki," alisema mwandishi mwenza wa ripoti ya utafiti huo Trevor Hamilton, ambaye ni mwanasayansi wa chuo hicho kikuu cha MacEwan nchini Canada,
Alisema samaki wanaweza kukumbuka kwamba sehemu maalum ina chakula bila kuwepo tishio la samaki wanaoweza kuwaua, na hivyo wataweza kurudi tena katika sehemu ile.
Wanasayansi hao wanasema samaki wakiwa baharini, ni muhimu waweze kutambua maeneo yalio na chakula ili waweze kuendelea kuishi.
Ili kupata Habari, Stori, na Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta PRINCE BEWISA, au
BONYEZA HAPA

TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?
Facebook Plugin by
princebewisa
Tags # MAAJABU & ASILI & TAKWIMU # MAKALA # TAFITI # UKWELI USIOEPUKIKA (FACTS) & NUKUU
Share This

About Benson Mmari
Benson Mmari ni mwaandishi wa makala za mitandaoni akijikita zaidi katika kuelimisha kuhusiana na masuala ya Afya, Saikolojia, na Mahusiano - Kimwili na kiroho.
Ni mwanateknolojia aliyebobea kwenye kazi zake tangu mwaka 2012.
Newer Article
TABIA HII MOJA ITAKUFANYA UWE MASIKINI MAISHA YAKO YOTE USIPOBADILIKA
Older Article
VINYWAJI VYA KUONGEZA NGUVU NA MADHARA YAKE KIAFYA
MADHARA YA KULA NYAMA NYEKUNDU
Benson MmariSept 18, 2017MAMBO YAKUANGALIA KIBIBLIA KWA MWANAMKE UNAYETAKA KUMUOA
Benson MmariSept 05, 2017WATU WENYE TABIA HIZI NI NGUMU SANA KUFANIKIWA
Benson MmariAug 21, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment