Post Top Ad
Monday, 21 August 2017

UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA ➞




« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »
Home
MAKALA
STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA
TAFITI
UCHUMI & BIASHARA
UJASIRIAMALI
UKWELI USIOEPUKIKA (FACTS) & NUKUU
WATU WENYE TABIA HIZI NI NGUMU SANA KUFANIKIWA
WATU WENYE TABIA HIZI NI NGUMU SANA KUFANIKIWA
Katika maisha wapo watu ambao ninaweza sema kwa jinsi ya sifa zao au kwa jinsi ya tabia zao walizonazo sio rahisi kufanikiwa. Hawa ni wale watu ambao tunasema ni aina ya watu ambao hawafanikiwi katika maisha yao.
Inawezekana ukawa huzijui sifa za watu hawa ambao hawafanikiwi katika maisha yao, lakini kupitia makala haya utajifunza sifa hizo za watu ambao kwa kiuhalisia huwa hawafanikiwi hata iweje, pengine wabadilike mara moja.
Najua hapo ulipo unataka kujua kwa hamasa kubwa watu ambao hawafanikiwi katika maisha yao huwa wana sifa zipi. Nami bila choyo yoyote, nakukaribisha bila hiana na twende kwa pamoja kujifunza sifa za watu ambao hawafanikiwi katika maisha.
1. Watu ambao kazi yao ni kulaumu na kulalamika.
Mara nyingi watu ambao ni walalamikaji sana, kufanikiwa kwao katika maisha huwa sio rahisi. Hili hutokea kwa sababu, husau majukumu yao ya msingi juu ya maisha yao na kuwapa wengine mzigo huo kwamba ndio wamesababisha maisha yawe hivyo.
Hata wewe ukiwa mtu wa kulalamika na kulaumu, utakuwa ni miongoni mwa watu ambao hawataweza kufanikiwa katika dunia hii, hadi pengine ubadilike. Ukifatilia, utaelewa vyema aina hii ya watu jinsi walivyowengi na wanakwama kweli.
2. Watu wanaojadili matatizo badala ya njia za kutatua matatizo.
Kama umekuwa ni mtu wa kujadili matatizo badala ya kutafuta njia za kutoka kwenye tatizo hilo, basi ni miongoni mwa watu ambao hawawezi kuja kufanikiwa katika maisha yao. Ili upate unachokitaka unatakiwa kujifunza kutatua changamoto na si kuzijadili. Kujadili changamo zako sana ni kujikwamisha mwenyewe.
3. Watu ambao hawataki kubadilika hata kama wanafanya makosa.
Wapo watu ambao ni wabishi na ambao maishani mwao ni kama wamegoma kubadilika kabisa. Hata watu hawa wakikosea bado kubadilika kwao ni kugumu sana. Hiyo haitoshi si watu wa kujifunza hata kidogo iwe kwenye vitabu au kupitia wengine. Pia watu hawa ni miongoni mwa watu ambao sio rahisi kuweza kufanikiwa.
4. Watu ambao ni watumwa kwa mambo yasio ya msingi.
Kuna watu ambao ni watumwa wa mambo yasiyo ya msingi ambayo kiuhalisia yanawarudisha nyuma sana kwenye maisha yao. Unapokuwa mtumwa sana pengine pombe kwa sana au wanawake ka wingi, unajitengenezea shimo la kushindwa kwako. Kwa lugha nyingine hivyo ni vitu ambavyo vinapoteza pesa ukiviendekeza vibaya.
5. Watu wanaojilinganisha sana na wengine.
Acha kufanya kosa la kujilinganisha na wengine kwenye maisha yako. Unapojilinganisha na wengine utashindwa kuwa bora pasipo kujua na mwisho wa siku utashangaa unakwama. Itakuwa badala ya kufanya mambo yako, unakua unakazana tu uwe kama fulani, hapo utakwama.
Hawa ndio watu ambao wana sifa nyingi za kutokufanikiwa katika maisha yao. Kama una sifa miongoni mwa hizo unabidi uwe makini sana ili na wewe usije ikafika mahali ukakwama na kubaki hapo. Jenga maisha yako makubwa ya kimafanikio kwa kujitahidi kutoka kwenye sifa hizo kama unazo.
Ili kupata Habari, Stori, na Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta PRINCE BEWISA, au
BONYEZA HAPA

TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?
Facebook Plugin by
princebewisa
Tags # MAKALA # STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA # TAFITI # UCHUMI & BIASHARA # UJASIRIAMALI # UKWELI USIOEPUKIKA (FACTS) & NUKUU
Share This

About Benson Mmari
Benson Mmari ni mwaandishi wa makala za mitandaoni akijikita zaidi katika kuelimisha kuhusiana na masuala ya Afya, Saikolojia, na Mahusiano - Kimwili na kiroho.
Ni mwanateknolojia aliyebobea kwenye kazi zake tangu mwaka 2012.
Newer Article
NJAA KUU 2 ZA WANANDOA NI HIZI
Older Article
MAMBO AMBAYO WATU WENYE MAFANIKIO HUFANYA
MADHARA YA KULA NYAMA NYEKUNDU
Benson MmariSept 18, 2017MAMBO YAKUANGALIA KIBIBLIA KWA MWANAMKE UNAYETAKA KUMUOA
Benson MmariSept 05, 2017WATU WENYE TABIA HIZI NI NGUMU SANA KUFANIKIWA
Benson MmariAug 21, 2017
Labels:
MAKALA,
STAILI ZA MAISHA & SAIKOLOJIA,
TAFITI,
UCHUMI & BIASHARA,
UJASIRIAMALI,
UKWELI USIOEPUKIKA (FACTS) & NUKUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment